Robertinho Awapiga Mkwara Ngoma na Onana

Hitimana Thiery aliwayewahi kuwa kocha wa Simba ameweka wazi kuwa ikiwa wachezaji wapya waliosajiliwa ndani ya kikosi cha Robertinho watashindwa kufanya vizuri kama ilivyokuwa kwa Saido Ntibanzokiza itaongeza presha kwao kutoka kwa mashabiki.

Robertinho Awapiga Mkwara Ngoma na Onana

Katika usajili wa dirisha kubwa Simba ilisajili wachezaji wa kimataifa na kitaifa ikiwa ni pamoja na Willy Onana, Fabrice Ngoma, Che Malone ambao hawa ni wakimataifa huku wazawa ikiwa ni Idd Chilunda, David Kameta (Duchu).

Thiery aliyewahi kuifundisha pia KMC na Namungo kwa nyakati tofauti, alibainisha kuwa wachezaji wote wapya wana kazi kubwa ya kufanya katika mechi za kitaifa na kimataifa.

“Kuna wachezaji ambao waliachwa na Simba hayo ni maamuzi ambayo wamefanya ila kwa wale wapya waliosajiliwa wanakazi kubwa kuonyesha kiwango iwe ni zaidi ya kile watangulizi wao walifanya.”

Robertinho Awapiga Mkwara Ngoma na Onana

Unaona mchezaji kama Saido Ntibanzokiza huyu baada ya kusajiliwa alionyesha kitu cha utofauti na wengi walikaa kimya kwa kuwa kazi ilionekana lakini ingekuwa tofauti hapo kungekuwa na maneno.

Hivyo wachezaji wale ambao wamesajiliwa na Simba kinachosubiriwa kwa sasa ni matokeo hilo wanapaswa kuelewa.  Alisema Thiery

Acha ujumbe