Kocha Mkuu wa Simba Mbrazili, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amefurahishwa na matokeo ya ushindi lakini amewataka wachezaji wake wacheze soka safi la pasi nyingi wakiwa wanamiliki mpira wao.

Simba katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara, walipata ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Mtibwa Sugar.
Odds kubwa kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni vitu vinavyoweza kubadilisha maisha yako kwa kukupatia pesa nyingi. Ingia mchezoni hapa.
Robertino alisema kuwa, bado vijana wake hawajacheza soka lile ambalo analolitaka, licha ya kupata ushindi mkubwa dhidi ya Mtibwa Sugar.
Robertino alisema kuwa anataka kuona wachezaji wake wakipiga pasi kutokea nyuma kwenda katika goli la wapinzani wao.

Aviator, poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Piggy Party na mingine kibao upige pesa na Meridianbet. Ingia www. meridianbet.co.tz.
Aliongeza kuwa anaamini vijana wake watacheza katika kiwango hicho bora anachokitaka wakati akiendelea kuwapa maelekezo katika uwanja cha mazoezi.
“Ni jukumu la mchezaji hivi kuona timu inafanya umiliki mzuri wa mpira kwa kupiga pasi sambamba na kufunga mabao mengi katika kila mchezo. Tunapata matokeo mazuri, lakini hatupigi pasi nyingi, hivyo tunatakiwa kuwapa burudani mashabiki wetu pamoja na kufunga mabao.”
Naendelea kufanyia kazi hilo katika uwanja cha mazoezi ili wachezaji wangu wafanye kile ambacho ninakitaka mimi,” alisema Robertinho.

