Konkoni Ashusha Presha ya Mabao Yanga

Mshambuliaji wa Yanga raia wa Ghana, Hafidh Konkoni amewaondoa wasiwasi mashabiki wa timu hiyo, kwa kutamka sasa hivi yupo fiti na tayari kuifungia mabao timu yake.

 

Konkoni Ashusha Presha ya Mabao Yanga

Konkoni ni kati ya washambuliaji wanaotegemewa katika kikosi cha timu hiyo, ambaye aliletwa kuchukua nafasi ya Fiston Mayele.

Nyota huyo akiwa na Yanga amecheza mechi moja pekee ya mashindano akitokea benchi katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba.

Konkoni alisema kuwa kwa muda ambao amekaa kambini Avic Town, Kigamboni Jijini Dar es Salaam unatosha kwake kuwapa furaha kwa kufunga mabao.

Konkoni Ashusha Presha ya Mabao Yanga

Konkoni alisema kuwa tayari ameshazoeana na wachezaji wake kwa sasa ambao amewakuta Yanga katika msimu huu, hivyo mashabiki watarajie makubwa katika michezo ijayo.

Aliongeza kuwa mashabiki wanatakiwa kutengeneza imani na yeye kwa sasa, kwani anafahamu kilichomleta Yanga.

“Sitakiwi kufananishwa na mchezaji yeyote ndani au nje ya Yanga, kikubwa nimepanga kufanya kile ambacho kimenileta hapa nilipo ambacho ni kufunga mabao pekee.”

Hadi sasa bado sijafanya kile ambacho ninataka kukifanya, sasa basi huu ni wakati wangu muafaka wa mimi kufunga baada ya kuwa tayari na fiti kucheza mechi.

Haitakuwa rahisi kwangu kufanya kitu kikubwa bila ya sapoti kubwa ya mashabiki ambao wanatakiwa kuniamini. Alisema Konkoni.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.