Klabu ya Simba ambayo ipo chini ya kocha mkuu Roberto Oliviera umemtangaza Mkurugenzi mpya ambaye ni Imani Kajula klabuni hapo ambaye anaenda kuchukua nafasi ya aliyekuwa C.E.O wa klabu hiyo Barbara Gonzalez.

Imani Majula amepewa mkataba wa miezi sita kuitumikia klabu hiyo ili kuona kama anaweza kuongeza kitu ndani ya klabu hiyo huku akiwa amebobea kwenye masuala mengine pia ukitoa soka.
Mwaka 1999-2003 Majula alikuwa ni meneja wa Masoko wa CRDB, kabla ya kuja kushika nyadhifa ya Mkrugenzi wa Masoko na Biashara Tanzania Postal Bank mwaka 2003-06, ndipo akawa tena Mkuu wa Masoko na Mawasiliano NMB mwaka 2006-2013.

Ndipo mwaka wa 2013 akawa Mkurugenzi wa EAG Grop, kwahiyo mpaka anajiunga na Wekundu wa Msimbazi alikuwa bado ni mkurugenzi.

