Al Hilal Kuanza na Namungo Hii Leo

Klabu ya Al Hilal kutoka Sudan ambayo kwasasa ipo nchini Tanzania inatarajia kucheza mchezo wake wa kirafiki hii leo dhidi ya Namungo FC kutoka Ruangwa mkoani Lindi.

 

Al Hilal Kuanza na Namungo Hii Leo

Al Hilal ambao ni wageni wa Simba walikuja nchini kwaajili ya kucheza michezo mitatu ya kujiandaa na michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika, ambapo kati ya michezo mitatu watakayocheza wa kwanza ni huu utakaowakutanisha dhidi ya Namungo FC.

Mchezo huo utapigwa majira ya saa 10:00 jioni  Chamazi Complex huku klabu ya Namungo ikitoka kupata kushinda kwa kishindo mchezo wake uliopita wakiwa ugenini dhidi ya Wanakino Boys.

Al Hilal Kuanza na Namungo Hii Leo

Mchezo huu wa leo utakuwa faida kwa timu zote mbili lakini sanasana kwa wageni Omdurman ambao wanatarajia kucheza mchezo wao wa kwanza kwenye makundi dhidi ya Mamelod Sundowns ya Afika Kusini.

Na mchezo wa pili watamenyana dhidi ya Al Ahly ya huko Misri hivyo kocha anataka kuona wapi apunguze na kuongeza ili kujua kuwa anaanzaje michuano hiyo na timu hizo kubwa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.