Keane: Rashford ni Mashine

Gwiji wa zamani wa Manchester United Roy Keane anasema mshambuliaji wa klabu hiyo anayefanya vizuri kwasasa Marcus Rashford anamuona kama mashine kwa namna anavyopambana.

Marcus Rashford ameonesha kumkuna mkongwe Roy Keane kutokana na ubora ambao amekua akiuonesha kwasasa ndani ya klabu hiyo. Mshambuliaji huyo mpaka ajiwa amefunga mabao 18 akiboresha kiwango mara dufu kutoka msimu uliomalizika.keaneMshambuliaji huyo amekua mchezaji anaeongoza kwa mabao tangu ligi zirejee kutoka kwenye kombe la dunia, Rashford amefanikiwa kufunga mabao 10 kwenye ligi tano bora ulaya na hii inaonesha namna amekua hatari msimu huu huku akiisaidi klabu yake ya Manchester United kuweza kupata matokeo katika michezo mbalimbali.

Keane ameendelea kusisitiza namna amefurahishwa na kuimarika kwa mshambuliaji huyo ambaye amedai ni kama mchezaji huyo ameweza kuvaa viatu vya Ronaldo vizuri kwani tangu kuondoka kwa Ronaldo klabuni hapo Rashford ameweza kuimarika na kufanya vizuri.keaneMshambuliaji Marcus Rashford ambaye alikua ana msimu mbaya sana mwaka 2021/22 akifunga mabao matano tu ndani ya msimu mzima, Lakini akiweza kuimarika kwa kiwango kikubwa ndani ya msimu huu 2022/23 ambapo mpaka sasa ameshafunga mabao 18 kwenye michuano yote.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.