Sneijder Anaamini Mourinho Bado ni Namba Moja

Staa wa zamani wa klabu ya Inter Milan na timu ya taifa ya Uholanzi Wesley Sneijder amesema anaamini kocha wa klabu ya As Roma Mreno Jose Mourinho bado ni namba moja duniani.

Jose Mourinho ambaye ametimiza miaka 60 katika maisha yake siku ya leo akiwa ndani ya klabu ya Roma, Huku akifanikiwa kuisaidia klabu hiyo kushinda taji la Uefa Conferernce League mwaka 2022 ambapo ilikua ni baada ya kupita miaka minggi bila klabu hiyo kushinda taji lolote.sneijderBaada ya kushinda taji la Uefa Conference League mwaka jana akiwa na klabu ya AS Roma alifanikiwa kuweka ekodi kwa kubeba kila taji ambalo lipo chini ya shirikisho la soka ulaya Uefa, Kwani alifanikiwa kubeba taji la ligi ya mabingwa ulaya akiwa na Fc Porto 2004, pamoja Inter Milan 2010, Uefa Europa 2017 akiwa na Manchester United na Uefa Conference League mwaka 2022 akiwa na As Roma.

Sneijder anamkumbuka zaidi Mourinho akiwa kama kocha wake ndani ya klabu ya Inter Milan mwaka 2010 wakifanikiwa kubeba mataji matatu ndani ya msimu mmoja, Huku staa huyo akiutafsiri kama msimu bora zaidi kwenye maisha yake ya soka na ndio sababu anaamini kocha huyo ni namba moja kwake.sneijderGwiji Wesley Sneijder ni miongoni mwa wachezaji waliunda Inter Milan dume kabisa nchini ya kocha ya kocha Jose Mourinho na kufanikiwa kushinda mataji matatu ndani ya msimu mmoja ambayo ni Ligi ya mabingwa barani ulaya, Ligi kuu ya Italia Serie A, na Copa Italia.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.