Klabu ya Simba inatarajia kuwakaribisha klabu ya Al Hilal nchini kesho ambao wanatarajia kuja kuweka kambi kwaajili ya kujiandaa na michuano ya Ligi ya Mabingwa na Wekundu hao ndio watakuwa wenyeji wao.

 

Simba Inatarajia Kuwakaribisha Al Hilal Nchini Kesho

Na timu hiyo kutoka Sudan wakiwa hapa nchini Tanzania watacheza michezo mitatu ya kirafiki ambapo watacheza dhidi ya Simba, Azam FC na Namungo.

Mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Al Hilal ndio utakuwa wa mwisho na utapigwa katika Dimba la Mkapa Februari 5, baada ya mchezo wa ligi ambapo vijana wa Roberto watakuwa wameshacheza dhidi ya Singida Big Stars.

Simba Inatarajia Kuwakaribisha Al Hilal Nchini Kesho

Baada ya mchezo huo Mnyama atasafiri kuelekea Guinea kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Horoya na baadae kurejea kwaajili ya mchezo wa pili ambao watamenyana dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco.

Wakati kwa Al Hilal wao watamenyana dhidi ya Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini ugenini, na baadae watamualika Al Ahly nyumbani kwao kwenye mchezo wa pili wa Klabu Bingwa.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa