Chiesa Aiomba Liverpool Imruhusu Arejee Italia

Mchezaji wa kimataifa wa Italia Federico Chiesa anaripotiwa kuwaomba Liverpool wamruhusu aondoke kwa mkopo mwezi Januari ili kupata muda zaidi wa kucheza, huku Milan, Roma na Napoli wote wakimtaka.

Chiesa Aiomba Liverpool Imruhusu Arejee Italia

Winga huyo alihamia Anfield majira ya joto kwa euro milioni 12 tu huku mkataba wake na Juventus ukidorora.

Miongoni mwa sababu kuu kwa nini Bianconeri hawakuwa tayari kumpa mkataba mpya ni rekodi yake mbaya ya majeraha na ambayo imeendelea nchini Uingereza.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amecheza mechi nne pekee za ushindani akiwa na jezi ya Liverpool kwa jumla ya dakika 123 uwanjani.

Chiesa Aiomba Liverpool Imruhusu Arejee Italia

Kwa kuzingatia hilo, Mirror Sport inathibitisha kuwa vinara wa EPL wako tayari kumruhusu Chiesa kuondoka kwa mkopo Januari ili apate nafasi zaidi ya kucheza.

Shida kubwa ni kwamba hakuna mtu nchini Italia aliye tayari kulipa hata nusu ya €7.5m kwa mshahara wa msimu, kwa hivyo Liverpool ingehitaji kusaidia kugawana mzigo.

Napoli, Milan na Roma ndio wanaovutiwa zaidi kumpa Chiesa muda wa kucheza msimu huu.

Acha ujumbe