Luis de la Fuente ameteuliwa kuwa kocha mpya wa Hispania, akichukua nafasi ya Luis Enrique ambaye ameachishwa kazi mapema leo.
Hispania iliondoka kwenye Kombe la Dunia Jumanne baada ya kushindwa kwa mikwaju ya penalti ya kushtukiza kutoka kwa Morocco huko Qatar. Mabingwa hao wa 2010 walishindwa kupata penati hata moja kufuatia kutoshana nguvu dakika 120.
Matokeo hayo ya kushtukiza yalitanguliwa na kampeni ya kundi la rollercoaster ambayo ilishuhudia ushindi wa 7-0 dhidi ya Costa Rica, sare ya 1-1 na Ujerumani na kufungwa 2-1 na Japan na kuwaacha washindi wa pili wa Kundi E.
Taarifa kutoka Shirikisho la Soka la Kifalme (RFEF) ilisema: “RFEF inapenda kumshukuru Luis Enrique na wakufunzi wake wote katika uongozi wa timu ya Taifa katika miaka ya hivi karibuni.”
Usimamizi wa michezo wa RFEF umehamisha kwa rais ripoti ambayo imedhamiriwa kwamba mradi mpya unapaswa kuanza kwa timu ya soka ya Hispania, huku lengo likiwa ni kuendelea na ukuaji uliopatikana katika miaka ya hivi karibuni kutokana na kazi iliyofanywa na Luis Enrique na washirika wake.
Taarifa hiyo haikuishia hapo pia RFEF imemchagua Luis de la Fuente kama kocha mpya wa Kitaifa, huku mechi yake ya kwanza itakuwa mwezi Machi wakati Hispania itaanza mechi za kufuzu kwa michuano ya Euro 2024 kwa michezo dhidi ya Norway na Scotland.
Luis de la Fuente aliifundisha Hispania na kupata ushindi katika mechi ya kirafiki dhidi ya Lithuania mnamo Juni 2021. Kocha huyo mpya ana miaka 61, na amepandishwa cheo kutoka nafasi yake ya awali kama bosi wa chini ya miaka 21 kuwaongoza vijana hao kutwaa ubingwa wa Ulaya 2019.
Pia aliiongoza Hispania kutwaa medali ya fedha katika Michezo ya Olimpiki ya 2020 jijini Tokyo, na kupoteza muda wa ziada kwa Brazil.
Luis De la Fuente ambaye alikuwa beki wa kushoto wa zamani wa Athletic Bilbao alichukua jukumu la kuinoa timu ya wakubwa kwa mechi ya kirafiki ya kujiandaa na michuano ya Euro 2020 dhidi ya Lithuania mnamo Juni 2021 wakati Luis Enrique alipokuwa akijitenga kwa sababu ya itifaki za Virusi vya Corona.
Akiwa mchezaji, alinyanyua taji la LaLiga mara mbili akiwa na Athletic pamoja na Copa del Rey mnamo 1984. Uamuzi wa RFEF unahitimisha muda wa Luis Enrique baada ya muda wa matumaini lakini wa kukatisha tamaa katika kuiongoza nchi yake.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 52 alichukua nafasi hiyo kwa mara ya kwanza Julai 2018 lakini alijiuzulu Julai iliyofuata kwa sababu za kibinafsi. Alirejea usukani mnamo Novemba 2019 na akasimamia mbio za Hispania hadi nusu fainali ya Euro 2020, ambapo pia walishindwa kwa mikwaju ya penalti, na ambao walikuwa mabingwa Italia.
Kiungo huyo wa zamani wa Real Madrid na Barcelona alilichezea Taifa lake mechi 62 kati ya 1991 na 2002, baada ya kukaa kwenye dimba la Roma na Celta Vigo, alirejea Camp Nou Mei 2014 na kushinda mataji tisa, ikiwa ni pamoja na matatu katika kampeni yake ya kwanza huko Catalonia.