Kwa mujibu wa jarida la Calciomercato imeripoti kuwa kocha wa Everton Rafael Benitez amewaambia viongozi wa klabu hiyo anahitaji mlinzi wa kati mwenye uzoefu mkubwa Katika eneo hilo kuelekea msimu ujao.
Benitez ameweka bayana anamuhitaji mlinzi wa klabu ya Napoli na timu ya Taifa ya Senegal Koulibaly (30) katika majira haya ya kiangazi.
Calciomercato imeweka bayana kuwa inaweza kuwa ngumu kwa Koulibaly kuelekea Everton kwakua mlinzi huyo anahitaji timu inayoshiriki mashindano ya klabu bingwa barani ulaya.
Bado uongozi wa Everton unaendelea kuwinda Saini ya mchezaji huyo na wapo tayari kuvunja benki kuhakikisha mchezaji huyo anatua katika klabu hiyo.
Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!
dorophina
Usajili ukianza msimu huu wa kiangazi patakuwa hapatoshi