Chelsea, Haaland Litakufa Jitu.

 

Taarifa kutoka London zimefichua dili la staa wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Norway, Erling Haaland, 20, kutua Chelsea dirisha hili linaweza kuwa gumu kutokana na sababu lukuki.

Chelsea imekuwa ikihusishwa kuwa karibu kuinasa saini yake hususan katika siku za hivi karibuni, lakini inaelezwa kwamba suala hilo linaonekana kuwa gumu.

Sababu mojawapo inayotajwa kufanya dili hilo lisifanikiwe ni kuondoka kwa Jadon Sancho aliyejiunga na Manchester United, hivyo Dortmund itakuwa ngumu kukubali kumuachia Haaland kwani timu yao itakuwa imepoteza makali eneo la ushambuliaji.

Mbali ya hilo, Chelsea inaweza ikakumbana na adhabu ya matumizi ya pesa nje ya utaratibu kutoka UEFA kwani ni msimu uliopita tu, imetumia kiasi kikubwa cha pesa kusajili mastaa kadhaa wakiwamo Kai Havertz na Timo Werner.

Lakini pamoja na hayo yote Chelsea wanajiandaa kumuongeza mshambuliaji wao Tammy Abraham kwenda upande wa pili katika dili hilo ili kupata saini ya Haaaland.


JIUNGE NA FAMILIA YA MABINGWA!

Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!

Italia, Italia Bingwa Euro 2020., Meridianbet

JIUNGE SASA!

2 Komentara

    Chelsea wakiamua uwaga awashindwi kitu

    Jibu

    Haaland akitua chelsea itakuwa poa sana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.