Dortmund Yawakingia Kifua The Blues

Pengine ni marudio ya yale yaliyotokea 2020 kwenye sakata la usajili wa Jadon Sancho. Borussia Dortmund wanaonesha ukomavu wao wa maamuzi sokoni.

Chelsea wamejikuta wakiambulia patupu kwenye dau lao la kwanza katika juhudi za kutaka kumsajili Erling Haaland kutoka BVB.

Tangu kusajiliwa kwa Kai Havertz na Timo Werner, The Blues wanahaha kumpata mshambuliaji mahiri atakayeiongoza timu hiyo kwani waliopo hawajafikia matarajio ya klabu hiyo.

Haaland ni miongoni mwa wachezaji wanaonyatiwa na vilabu vingi barani Ulaya. Japokuwa mchezaji mwenyewe anandoto za kucheza Real Madrid, anahusishwa na Man United, Man City na Chelsea kwenye dirisha hili la usajili.

Imeripotiwa kuwa, Chelsea walitoa kiasi cha pesa sambamba na mchezaji mmoja kati ya Callum Hudson-Odoi na Tammy Abraham kama sehemu ya dau la kumsajili Haaland. Hata ivyo, Dortmund wamewakataa Chelsea mchana kweupe!

Bado haijajulikana kama BVB watachukua uamuzi wa kumuuza Haaland na Sancho wote katika dirisha moja au watasimamia msimamo wao wa kutomuuza Haaland msimu huu ikiwa ni tayari wameshamuuza Sancho kwenda United.


JIUNGE NA FAMILIA YA MABINGWA!

Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!

Italia, Italia Bingwa Euro 2020., Meridianbet

JIUNGE SASA!

2 Komentara

    Hiyo bonus naweza kuichezea kupitia account yangu

    Jibu

    Nasubilia usajili kwa hamu kubwa maana ni itakuwa balaa

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.