Kocha mkuu wa Chelsea Graham Potter amesema kuwa kiwango cha mchezaji wake Raheem Sterling kitaimarika  ikiwa Chelsea itapiga hatua mbele kwani kwasasa bado haijakaa sawa kutokana na matokeo wanayoyapata.

 

Potter Ameapa Kwamba Kiwango cha Sterling Kitaimarika.

Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Uingereza amekuwa na shida ya kufunga mabao tangu ahamie kutoka Manchester City hadi Stamford Bridge kabla ya kampeni ya sasa, huku winga huyo akitafuta kuimarisha nafasi yake katika mipango ya kocha wa Uingereza Gareth Southgate.

Huku mchezaji mwenzake wa klabu na timu ya Kimataifa Reece James akiwa amepata jeraha ambalo litamfanya akae nje kwa muda mrefu huku taarifa zingine zikisema kuwa huenda akakosa Kombe la Dunia, na hivyo kumfanya acheze eneo la James.

Lakini Potter amependekeza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 atarejea katika kiwango kizuri endapo  wachezaji wanaomzunguka pia watapiga hatua mbele. Alsema kuwa;

Potter Ameapa Kwamba Kiwango cha Sterling Kitaimarika.

“Ni jambo ambalo tunapaswa kuliangalia sio kwa kukaribia mtu mmoja bali kama timu. Tunaweza kufanya vizuri zaidi lakini tukifanya vizuri zaidi kama timu, basi watu binafsi watanufaika na hilo kwa hiyo hapo ndipo kazi ilipo.”

Potter amekiri kuwa mchuano unaokuja huenda ukawa na athari kwa wachezaji kwani wanalenga kuepusha maswala yoyote ambayo yanaweza kuwazuia kugombana, lakini Potter anasema kuwa hadhani kama hiyo inaathiri uchezaji wao kwani wao ni wanadamu pia.

Chelsea wanatarajiwa kushuka dimbani hapo kesho kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa kucheza dhidi ya Salzburg ambapo mechi ya kwanza walitoa sare lakini The Blues ndio wanaongoza kundi hilo wakiwa na pointi 7.

Potter Ameapa Kwamba Kiwango cha Sterling Kitaimarika.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa