Potter Asema Manchester United Ilistahili Pointi Dakika za Lala Salama

Kocha mkuu wa klabu ya Chelsea Graham Potter amesema kuwa Manchester United ilistahili kupata alama moja hapo jana kwenye mchezo uliomalizika kwa sare ya 1-1, huku Mashetani Wekundu walipokuwa ugenini dhidi ya The Blues.

 

Potter Asema Manchester United Ilistahili Pointi Dakika za Lala Salama

Vijana wa Potter ndio ambao walianza kupata bao katika kipindi cha pili dakika za 80s kwa mkwaju wa penati baada ya mchezaji wa United kumchezea rafu mshambuliaji wa Chelsea Armando Broja kisha mkwaju huo ukatupiwa kambani na Jorginho.

Baada ya kuongezwa dakika 6 za nyongeza United walikuwa wakilisakama lango la The Blues na hatimaye wakapata bao la kusawazisha dakika ya 94, kupitia kwa kiungo wao Casemiro na hivyo kufanya mchezo kumalizika kwa sare ya moja kwa moja.

Baada ya mchezo kumalizika kocha wa The Blues Potter alisema kuwa timu yake haikujituma vya kutosha kupata pointi tatu na vijana wa Ten Hag walistahili kupata alama moja.

Potter Asema Manchester United Ilistahili Pointi Dakika za Lala Salama

Aliendelea kusema kuwa hawezi kusimama na kusema kuwa walistahili ushindi, timu zote mbili zilijitahidi. Unapofunga kwa kuchelewa kama unavyofanya kuna hisia kwamba umepoteza pointi lakini katika muda wa mchezo, pointi ni sawa.

Chelsea sasa wamecheza mechi tano mfululizo na United na ni  mechi ambayo ina sare nyingi zaidi katika historia ya Ligi kuu ya Uingereza ambapo wana jumla ya sare 26, huku jana Blues Kepa akiokoa mipira hatari langoni kwake kutokana na ubora wake.

“Nilidhani tungeweza kushambulia vizuri zaidi wakati fulani. Tulikuwa na nafasi, walikuwa na nafasi, kwa hivyo hatua ni sawa.”

Potter Asema Manchester United Ilistahili Pointi Dakika za Lala Salama

Chelsea mechi inayofuata ni ya Ligi ya Mabingwa ambapo watakuwa ugenini kucheza dhidi ya FC Salzburg huku mechi ya kwanza wakitoshana nguvu na The Blues ndio wanaongoza kundi hilo wakiwa na pointi 7.

Acha ujumbe