Potter Juu ya Mkataba wa N'golo Kante

Kocha mkuu wa Chelsea Graham Potter ameongea kuhusu mkataba wa kiungo wa timu hiyo  N’Golo Kanté ambapo mkataba wake unamalizika mwezi Juni huku bado kukiwa hakuna mwafaka wa mchezaji huyo na timu yake.

 

Potter Juu ya Mkataba wa N'golo Kante

Potter amesema kuwa jambo zuri kwasasa ni kumsaidia kuwa fiti na bado kiungo huyo ana safari ndefu ya kwenda mbeleni .

Kocha huyo ambaye mpaka sasa hajapoteza mchezo wa aina yoyote amesema kuwa lazima wahakikishe mchezaji huyo anapata matibabu sahihi wakati anafurahia soka lake na pia wanaweza kufikiria kuhusu mkataba wake.

Potter Juu ya Mkataba wa N'golo Kante

Kante ambae ni mshindi wa  Kombe la Dunia mwaka 2018 na timu yake ya Ufaransa, taarifa za mwanzo zilisema kuwa anahitaji mkataba mrefu kwani Koulibaly ana mkataba mrefu kwanini yeye asipewe mkataba huo.

The Blues wanasita kutoa mkataba mrefu kwa kiungo huyo kutokana na umri wake kuwa mkubwa miaka 30 si haba lakini pia kupata majeraha ya hapa na pale yanachangia pia timu hiyo kuhofia kumpa mkataba mrefu halafu aumie.

Potter Juu ya Mkataba wa N'golo Kante

The Blues leo, watakuwa nyumbani Stamford Bridge kuwaalika Manchester United ya Erik Ten Hag huku msimu uliopita kwenye ligi waligawana pointi moja moja mechi zote mbili.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.