Kocha wa Manchester Eric Ten Haag amefunguka kua pamoja na yote yaliyotokee lakini staa wa klabu hiyo Cristiano Ronaldo anabaki kua mchezaji muhimu kwenye kikosi chake.
Kocha huyo ameyazungumza hayo wakati akihojiwa kuhusu kuingia sokoni Januari na kusajili mshambuliaji mpya huku yeye akisisitiza hataingia sokoni Januari kwani ana mshambuliaji kariba ya Ronaldo klabuni hapo hivo hataingia sokoni kutafuta mchezaji mwingine.
“Ninamtegemea Ronaldo bado.Kwa kilichokea sio kitu sana” Ten Haag alipoulizwa kuhusu kusajili mshambuliaji mwezi Januari huku msimamo wake ukiwa bado anamuhesabu staa huyo kama mchezaji muhimu kikosini.
Kocha Ten Haag pia ameonekana ni kocha mwenye kusimamia misingi na nidhamu ya kazi kwani licha ya ukubwa wa Ronaldo lakini amempa adhabu na kumuonesha namna anatakiwa kuishi kwenye klabu kama kiigizo chema kwa vijana wadogo.
Manchester United ambayo imesafiri mpaka jijini London kwenda kumenyana na klabu ya Chelsea ambapo staa huyo atakosekana kutokana na adhabu aliyipata baada ya kuonesha utovu wa nidhamu katika mchezo wa katikati ya wiki dhidi Tottenham Hotspurs.

