Klabu ya Azam Fc ipo mbioni kumtimua kocha wake mkuu Dennis Lavagne raia wa Ufaransa baada ya kupata matokeo ya kutoridhisha hivi karibuni na kushindwa kufikia malengo ya klabu hiyo.
Taarifa za ndani kutoka klabu ya Azam zinaeleza klabu hiyo ipo kwenye hatua za mwisho kuvunja mkataba na kocha huyo ambaye alitambulishwa mwanzaoni mwa mwezi wa tisa na kufikia mwezi wa kumi anakaribia kufungashiwa virago.
Kocha huyo ameiongoza klabu ya Azam Fc katika michezo minne ya ligi kuu akifungwa miwili na kushinda miwili huku akitolewa kwenye michuano ya kombe la shirikisho Afrika na viongozi wa klabu hiyo kuona kocha Lavagne hawezi kuwafikisha nchi ya ahadi.
Azam Fc ambao wamepoteza mchezo jana kwa kufungwa na klabu KMC inaelezwa ndo sababu kubwa kwa viongozi wa klabu hiyo kutaka kusitisha mkataba wa kocha huyo.
Taarifa zinaeleza timu hiyo itabakichini ya kocha Badru pamoja Kali Ongala ambae ni kocha wa washambuliaji wa klabu hiyo.

