Kiungo wa zamani wa Real Madrid Guti amesema kuwa iwapo Kylian Mbappe atajiunga na Real Madrid, lazima ainamishe kichwa chini kutokana na kile kilichotokea wakati akihusishwa kujiunga na timu hiyo.

 

Guti Amuonya Mbappe Kuwa Mpole Iwapo Atajiunga na Real Madrid

Nyota huyo wa Paris Saint-Germain amekuwa akihusishwa na kuhamia Santiago Bernabeu, lakini aliipuuza Madrid mwaka jana alipokubali kusaini mkataba mpya katika mji mkuu wa Ufaransa.


Ripoti zinaendelea kupendekeza uhamisho katika miaka michache ijayo bado unawezekana, licha ya Madrid kughadhabishwa na uamuzi wa Mbappe ambao uliwazuia kuweza kumsajili kwa uhamisho wa bure mwishoni mwa msimu uliopita.

Akiongea kwenye El Chiringuito, Guti alisema: “Mbappe lazima aje Real Madrid akiwa ameinamisha kichwa na kuwa kama mmoja wa wengine kwenye chumba cha kubadilishia nguo. Kama si hivyo amekosea na hajui anawakilisha klabu gani. Ni kweli Luis alikuja, Ronaldo akaja…”

Guti Amuonya Mbappe Kuwa Mpole Iwapo Atajiunga na Real Madrid

Kiungo huyo ameongeza kuwa hajui ukweli wake ukoje huko Paris na jinsi inavyoendelea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo vya PSG. Anaweza kuwa mchezaji bora zaidi duniani ambaye angesajiliwa, lakini Real Madrid ni zaidi ya hapo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amefunga mabao 27 katika mechi 28 alizochezea PSG msimu huu na hivi karibuni amekuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kufunga mabao 150 kwenye Ligue 1 kwa miaka miwili.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa