Klabu ya soka ya Simba imetangaza wachezaji wake 24 ambao itasafiri nao leo kuelekea nchini Uganda kwajili ya mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya klabu ya Vipers.
Simba wanakwenda nchini Uganda wakiwa na kikosi chao chote kwenda kumenyana na klabu ya Vipers katika mchezo huo utakaopigwa siku ya jumamosi nchini Uganda, Klabu hiyo ya wekundu wa msimbazi inakwenda nchini Uganda kwajili ya kutafuta ushindi katika mchezo wao wa kwanza wa ligi ya mabingwa Afrika.Wekundu wa Msimbazi watakwenda Uganda wakiwa na rekodi mbaya baada ya kupoteza michezo yao miwili awali ya ligi ya mabingwa Afrika, Hivo mchezo dhidi ya Vipers utakua ni mchezo muhimu zaidi kwa Wekundu wa Msimbazi kwani inaweza kuamua hatma yao kwenye michuano hiyo.
Klabu Simba ambayo imekua na rekodi nzuri kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Afrika na kufanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali mara tatu ndani ya miaka mitano, Lakini msimu huu hali inaonekana kua mbaya mpaka wakati kwani wamepoteza michezo miwili ya awali.Simba mpaka sasa wanaonekana hawajakaa sawa baada ya kutokupata matokeo katika michezo yao mitatu ya mwisho katika mashindano yote, Mchezo dhidi ya Vipers siku ya jumamosi utaweza kufufua matumaini mapya ya wao kuweza kufuzu hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa ulaya.