Klabu ya soka ya Simba leo itashuka dimbani kuwakaribisha matajiri wa jiji la Dar-es-salam klabu ya Azam katika mchezo wa ligi kuu ya NBC utakaopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa.
Klabu ya Simba itakua inajitafuta katika mchezo huo baada ya kutoka kupokea kichapo kizito katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kufungwa mabao matatu kwa bila katika uwanja wa Benjamin Mkapa dhidi ya Raja Casablanca, Hivo mchezo wa leo dhidi ya Azam utakua muhimu kwa timu hiyo kueza kurudidsha kujiamini kwao kuelekea michezo mingine.Wekundu wa Msimbazi watashuka dimbani kukabiliana na Azam wakiwa na kumbukumbu za kupoteza mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya NBC, Hivo mchezo wa leo pia utakua wa kisasi kwa upande wa Wekundu wa Msimbazi kwani watahitaji kuifunga Azam ili kulipiza kisasi.
Simba wakiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya NBC wakiwa nyuma kwa alama sita dhidi ya vinara klabu ya Yanga, Mchezo wa leo pia utakua na umuhimu zaidi katika kupunguza pengo la alama baina yao na vinara klabu ya Yanga.Vilabu vya Simba na Azam vimekua na upinzani mkali kwa muda mrefu sasa lakini Wekundu wa Msimbazi wanaonekana kutawala zaidi katika matokeo baina ya timu hizo, Azam wao watajaribu kufanya ambacho walifanya katika mchezo wa kwanza katika dimba la Benjamin Mkapa.