Klabu ya Liverpool leo watakua nyumbani kuwakaribisha klabu ya Real Madrid katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya hatua ya 16 bora mchezo ambao unatazamiwa kua mchezo wa kisasi baina ya vilabu hivo.

Klabu ya Liverpool itakua ni na nafasi ya kulipa kisasi kw akile klichotokea mwezi Mei mwaka jana baada ya kupoteza mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa ulaya, Klabu ya Real Madrid ilifanikiwa kuifunga klabu ya Liverpool bao moja kwa sifuri katika mchezo wa fainali.LiverpoolReal Madrid itakwenda kumenyana na Vijogoo wa Anfield ambao wanaonekana kama wameanza kurejea kwenye ubora baada ya kushinda michezo miwili mfululizo, Real Madrid wao nao watakua bado wanajitafuta kwenye mchezo huo baada ya kutokua na matokeo mazuri baada ya michuano ya kombe la dunia.

Liverpool wamekua hawafanyi vizuri kwenye msimu huu haswa kwenye ligi kuu ya Uingereza lakini siku za karibuni wameonekana wameanza kurejea kwenye ubora wao, Huku wachezaji wao muhimu ambao walikua wamepata majeraha wameanza kurejea kwenye kikosi.LiverpoolKlabu ya Real Madrid wao wamesafiri mpaka jijini Liverpool wakiwa na timu yao nzima, Lakini mabingwa hao watetezi watawakosa baadhi ya nyoota wao wawili kwenye eneo la katikati ya kiwanja ambao wamekua mhimili kwenye timu hiyo Toni Kroos pamoja na Aurelien Tchouameni ambao wamepata majeraha na kushindwa kusafiri na timu.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa