Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Borussia Dortmund Karim Adeyemi amepata majeraha ya misuli katika mchezo wa ligi kuu ya Ujerumani dhidi ya Hertha Berlin na anatarajiwa kuukosa mchezo wa marudioano dhidi ya Chelsea.
Mchezaji Karim Adeyemi ambaye ndie mfungaji wa bao pekee katika mchezo wa awali ulipigwa katika dimba la Signal Iduna Park ambapo Chelsea walipokea kichapo cha bao moja kwa bila, Imetaarifiwa atakosekana katika mchezo wa marudiano kati ya klabu ya Borussia Dortmund dhidi ya Chelsea.Mchezaji huyo anatarajiwa kua nje ya uwanja kwa wiki tatu mpaka nne kutokana na majeraha ya misuli ambayo ameyapata na kumfanya kushindwa kumaliza mchezo kati ya Borussia Dortmund na klabu ya Hertha Berlin, Kutokana na mchezaji huyo kukosekana uwanjani kwa wiki tatu au nne ni wazi atauokosa mchezo wa Chelsea ambao unapigwa wiki ijayo.
Klabu ya Chelsea itakua imepata ahuaeni kidogo baada ya kusikia taarifa hizo kwani mchezaji huyo ni moja kati ya wachezaji mahiri ndani ya klabu ya Dortmund na alifanikiwa kuisumbua zaidi safu ya ulinzi ya Chelsea katika mchezo wa awali uliopigwa Signal Iduna Park.Karim Adeyemi ambaye atakosekana katika mchezo wa marudiano kati ya Chelsea na Dortmund ni wazi klabu ya Borussia Dortmund itakua kwenye wakati mgumu, Kwani mchezaji huyo mwenye miaka 21 tu amekua moja ya wachezaji wenye mchango mkubwa ndani ya klabu ya Borussia Dortmund.