Hakimi Afikishwa Mahakamani Kujibu Tuhuma za Ubakaji

Mchezaji wa Paris Saint-Germain FC, Achraf Hakimi, ameagizwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma za ubakaji zinazodaiwa kutokea Februari 2023. Ofisi ya mwendesha mashtaka ya Nanterre pamoja na wakili wa mchezaji huyo wamethibitisha kuwa raia huyo wa Morocco atashtakiwa rasmi mbele ya mahakama ya jinai ya Hauts-de-Seine.

Hakimi Afikishwa Mahakamani Kujibu Tuhuma za Ubakaji

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vya Ufaransa na Uingereza, Hakimi anatuhumiwa kumbaka mwanamke mwenye umri wa miaka 24 katika makazi yake eneo la Boulogne-Billancourt, karibu na Paris, Februari 25, 2023. Baada ya madai hayo, uchunguzi ulifunguliwa na waendesha mashtaka wa Nanterre, na sasa kesi imeamuliwa kupelekwa mahakamani.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kupitia ujumbe aliouchapisha katika mtandao wa X, Hakimi amekanusha vikali tuhuma hizo, akisema kuwa ni za uongo na anaamini kuwa ukweli utawekwa wazi mahakamani. “Leo hii, shtaka la ubakaji linatosha kupelekea kesi mahakamani hata kama ninapinga na kila kitu kinaonesha kuwa ni uongo. Ninasubiri kesi hii kwa utulivu ili ukweli ujulikane hadharani,” ameandika.

Hakimi Afikishwa Mahakamani Kujibu Tuhuma za Ubakaji

Wakili wake, Fanny Colin, naye ameeleza kuwa kesi hiyo inategemea ushahidi wa upande mmoja pekee, akidai kuwa mlalamikaji hakushirikiana kikamilifu katika baadhi ya vipimo na uchunguzi uliopendekezwa. Hata hivyo, mamlaka za sheria zimeendelea na mchakato wa kisheria ili mahakama iweze kusikiliza na kuamua suala hilo.

Katika mahojiano ya awali na kituo cha televisheni cha Ufaransa, Hakimi alieleza kuwa tukio hilo limekuwa pigo kubwa kwake na familia yake, akisisitiza kuwa hana hatia na yuko tayari kushirikiana na vyombo vya dola ili ukweli ujulikane.

Hakimi Afikishwa Mahakamani Kujibu Tuhuma za Ubakaji

Kesi hiyo sasa itasikilizwa rasmi mahakamani, ambapo pande zote zitapata nafasi ya kuwasilisha ushahidi wao huku macho ya wadau wa soka na umma yakifuatilia kwa karibu mwenendo wa shauri hilo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.