Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amesema kuwa beki wake  Pablo Mari anaendelea vizuri na hajaumia sana baada ya kuchomwa kisu huko Milan, huku mchezaji huyo kwasasa akiwa anaitumikia Monza kwa mkopo akitoka The Gunners.

 

Arteta: Mari Anaendelea Vizuri Baada ya Kuchomwa Kisu Huko Milan.

Beki huyo wa kati wa Brazil alikuwa mmoja wa watu kadhaa waliojeruhiwa katika matukio ya kutatanisha katika duka kubwa la Carrefour, huku klabu ambayo aliyopo sasa inayoshiriki Serie A kuthibitisha baadae.

Arteta, ambaye timu yake imepoteza mechi ya kwanza katika mechi ambazo amecheza kwenye Ligi ya Europa dhidi ya PSV, huku kjocha huyo akitoa maoni mafupi alipozungumza na vyombo vya habari baada ya mchezo.

Arteta: Mari Anaendelea Vizuri Baada ya Kuchomwa Kisu Huko Milan.

Arsenal walitoa taarifa, wakieleza kuwa wamewasiliana na wakala wa Mari na wamesikitishwa na kushtukishwa kusikia habari mbaya kuhusu mchezaji huyo kuchomwa kisu nchini Italia na kuwaweka watu kadhaa hospitalini akiwemo beki wao wa kati. Aliongeza kwa kusema kuwa;

“Tumekuwa tukiwasiliana na wakala wa Pablo ambaye ametuambia yuko hospitali na hajaumia sana. “Mawazo yetu yako kwa Pablo na waathiriwa wengine wa tukio hilo baya.”

Arteta: Mari Anaendelea Vizuri Baada ya Kuchomwa Kisu Huko Milan.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa