Conte Afungiwa Mechi 2 na Kutozwa Faini Baada ya Kuonyeshwa Kadi Nyekundu Dhidi ya Inter

Kocha wa Napoli, Antonio Conte, amepigwa marufuku ya mechi mbili katika Serie A na kutozwa faini ya euro 15,000 baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa ugenini dhidi ya Inter siku ya Jumapili.

Conte Afungiwa Mechi 2 na Kutozwa Faini Baada ya Kuonyeshwa Kadi Nyekundu Dhidi ya Inter

Conte hataiongoza Napoli akiwa kando ya uwanja katika mechi mbili zijazo dhidi ya Parma na Sassuolo, baada ya adhabu hiyo ya kufungiwa mechi mbili kufuatia kadi nyekundu aliyopata kwenye mchezo wa Jumapili dhidi ya Inter.

Katika mchezo huo wa Jumapili, Conte alipoteza utulivu kipindi cha pili baada ya Inter kupewa penalti kufuatia ukaguzi wa VAR. Kocha huyo wa Napoli alipiga mpira akiwa kwenye mstari wa pembeni, jambo lililosababisha aonyeshwe kadi nyekundu. Kabla ya kuondoka uwanjani, alirusha chupa chini na kumpigia kelele afisa wa nne kwa hasira.

Napoli watarudi uwanjani leo katika mchezo wa kiporo wa raundi ya 16 dhidi ya Parma nyumbani. Jumamosi ijayo, watakutana na Sassuolo, pia kwenye Uwanja wa Stadio Maradona.

Meridianbet inakwambia kuwa endelea kubashiri hapa kwani ODDS KUBWA na machaguo zaidi ya 1000 yapo hapa. Ingia kwenye akaunti yako na uanze safari yako ya ushindi sasa.

Conte Afungiwa Mechi 2 na Kutozwa Faini Baada ya Kuonyeshwa Kadi Nyekundu Dhidi ya Inter

Katika raundi hiyo ya mwisho ya Serie A, makocha Paolo Vanoli wa Fiorentina na Davide Nicola wa Cremonese nao walionyeshwa kadi nyekundu, lakini walipewa adhabu ya kufungiwa mechi moja pekee.

Mlinzi wa Lecce, Enilive Gaspar, amefungiwa mechi tatu, huku Nicolò Cambiaghi wa Bologna akikosa mechi mbili zijazo kutokana na tabia ya vurugu.

Wachezaji waliopigwa marufuku ya mechi moja ni Lameck Banda (Lecce), Antonio Caracciolo (Pisa), Juan Jesus (Napoli), Giuseppe Pezzella (Cremonese), Ylber Ramadani (Lecce) na Nicolò Zaniolo (Udinese).

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.