Thiago Motta anathibitisha kuwa hatajiuzulu baada ya Juventus kupoteza 3-0 dhidi ya Fiorentina akisema kuwa ‘itakuwa rahisi sana.’

Bianconeri walipata kipigo cha pili mfululizo kwenye Uwanja wa Stadio Franchi siku ya jana. Miamba hao wa Serie A wameruhusu mabao saba katika mechi mbili zilizopita, bila kufunga hata moja, na ushindi wa Bologna dhidi ya Lazio uliisukuma Juventus nje ya nne bora.
Mkurugenzi wa Juventus Cristiano Giuntoli alisema Motta hatafukuzwa kazi, na bosi wa Bibi Kizee huyo alisema hatajiuzulu.
“Itakuwa rahisi sana kufanya hivyo, na sipendi mambo rahisi. Tunahitaji kushinda, inabidi tutafute mbinu ya kupata pointi tunazohitaji ili kufikia lengo letu ambalo ni kumaliza katika nafasi nne za juu za ligi.” Motta aliiambia DAZN kupitia TMW.
Thiago Motta aliendelea kuelezea kupoteza kwa pili mfululizo kwa Juventus akisema kuwa ni kama muendelezo wa mechi iliyopita, hadithi sawa.


