Liverpool v Newcastle United EFL Cup 16/03/2025. Cup Final Fabian Schar 5 of Newcastle United clerks the ball away from Federico Chiesa 14 of Liverpool during the EFL Carabao Cup Final match between Liverpool and Newcastle United at Wembley Stadium, London, England on 16 March 2025. London Wembley Stadium Greater London England Editorial use only DataCo restrictions apply See www.football-dataco.com , Copyright: xGrahamxHuntx PSI-21648-0135
Federico Chiesa aliifungia Liverpool, lakini Newcastle ya Sandro Tonali ilishinda Kombe la EFL kwenye Uwanja wa Wembley, na kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Reds.
Mchezaji wa kimataifa wa Italia Tonali ameshinda kombe lake la kwanza nchini Uingereza. Timu yake ya Newcastle iliilaza Liverpool 2-1 Uwanja wa Wembley jana kwenye Fainali ya Kombe la EFL, ikiwa ni zawadi yao ya kwanza katika kipindi cha miaka 56.
Tonali alianza mchezo kwa Magpies na kucheza dakika zote 90, akipata kadi ya njano katika dakika za lala salama.
Dan Burn aliipatia Magpies bao la kuongoza dakika ya 53 kabla ya kipindi cha mapumziko, huku Alexander Isak akifunga bao la pili dakika ya 53.
Winga wa Liverpool Chiesa alitambulishwa dakika ya 74 na kuzifumania nyavu kwenye dakika za majeruhi, lakini haikutosha kuwasaidia Reds kurejea.
Chiesa tayari alikuwa amefunga mabao mawili kwenye uwanja wa Wembley akiwa na timu ya taifa ya Italia kwenye michuano ya Euro 2020.
Chiesa sasa amefunga mabao mawili katika mechi 11 akiwa na Liverpool, huku Tonali akiwa na wakati mzuri zaidi Newcastle, akifunga mabao matatu na kutoa asisti mbili katika mechi 34 katika michuano yote.