Federico Valverde Asaini Mkataba Mpya Madrid

Kiungo wa klbu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Uruguay Federico Valverde amefanikiwa kusaini kandarasi mpya ndani ya klabu hiyo itakayomueka ndani ya timu hiyo mpaka mwaka 2029.

Federicco Valverde alikua ana mkataba ndani ya klabu hiyo lakini Ral Madrid wameamua kumuongezea mkataba kiungo huyo mpaka mwaka 2029 kwajili ya kujenga kikosi cha muda mrefu kitakacholeta ushindani.federico valverdeReal Madrid wanataka kutengeneza kizazi kipya cha dhahabu ambacho kitaweza kutawala soka la ulaya kama kizazi kilichopita, Ikiwa ndio sababu ya kusainisha mikataba ya muda mrefu wachezaji vijana.

Mpaka sasa Real Madrid imeshahakikisha inawaongezea mikataba wachezaji wake vijana kama Eduardo Camavinga, Rodrygo Goes, Vinicius Jr,na sasa kiungo huyo wa kimataifa wa Uruguay mwenye miaka 23.federico valverdeKiungo Federico Valverde amekua na kiwango bora tangu apewe nafasi kwa mara ya kwanza klabuni hapo akitokea timu ya vijana ya klabu hiyo maarufu kama Castilla, Huku mpaka sasa ameendelea kua mchezaji muhimu jambo lilivutia uongozi wa klabu hiyo.

Acha ujumbe