Kiungo wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Uruguay Federico Valverde anatarajiwa kuongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo muda mrefu zaidi.
Federico anatarajiwa kuongeza mkataba mpya utakaomuweka klabuni hapo mpaka mwaka 2028, Klabu ya Real Madrid ipo kwenye mchakato wa kuwaongezea mikataba wachezaji wake muhimu klabuni hapo.Kiungo huyo wa kimataifa wa Uruguay ni miongoni mwa wachezaji muhimu kwasasa ndani ya kikosi cha Real Madrid, Klabu hiyo inafahamika inataka kuandaa mradi wa muda mrefu ambao utajengwa na vijana wadogo na ndio sababu wanawaongezea mikataba wachezaji vijana klabuni hapo.
Real Madrid imeanza kujiandaa na kuondoka kwa utatu wao wa viungo wa katikati uliokua ukiundwa na Toni Kroos, Luca Modric, na Casemiro ambaye aliondoka msimu uliomalizika ambapo viungo wote hao wameshatafutiwa mibadala klabuni hapo.Kiungo Federico Valverde amekua akifanya vizuri ndani ya klabu ya Real Madrid tangu alipopewa nafasi akitokea timu ya vijana ya klabu hiyo inayofahamika kama Castilla, Hivo kutokana na kiwango chake Real Madrid imeonesha kuvutiwa kuendelea kubaki nae kwa muda mrefu.