Kiungo wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Uruguay Federico Valverde anaota kua nahodha wa klabu hiyo siku moja kwakua ni jambo ambao litamfanya ajiskie vizuri.
Federico Valverde anaamini anaweza kuja kua nahodha wa klabu hiyo kubwa kabisa ulimwenguni, Kiungo huyo amekua akionesha ubora mkubwa sana ndani ya klabu hiyo tangu amepewa nafasi kwa mara ya kwanza.Kiungo huyo pia amewazungumzia manahodha wa klabu hiyo kwasasa kama Dani Carvajal, Luca Modric, na Toni Kroos na kusema anajifunza mambo mengi kwao kwakua ni kioo.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Uruguay ambaye ametoka timu ya vijana ya klabu ya Real Madrid maarufu kama Castilla ni mchezaji ambaye amekua akionesha ubora wa juu, Lakini pia ameonesha ana haiba ya uongozi ndani yake.Federico Valverde bado anasisitiza kua nahodha wa klabu hiyo kubwa kabisa ulimwenguni ni ndoto yake huku akieleza kama mtu ambaye anaamini ndoto hiyo itafanikiwa, Kwani hii inakua mara ya pili kwa kiungo kusema anatamani kuja kua nahodha wa Real Madrid.