Manula Arejea Mazoezini na Wenzake

Golikipa wa klabu ya Simba Aishi Salum Manula amerejea mazoezini na kikosi cha kwanza cha timu hiyo baada ya kukaa nje ya uwnaja kwa muda mrefu akiuguza majeraha yake.

Manula leo ameonekana katika viwanja vya Bunju ilipo kambi ya klabu hiyo pamoja na uwanja wa mazoezi wa klabu ya Simba akiwa anajifua na wenzake ikiwa ni mara ya kwanza tangu apate majeraha ndani ya klabu hiyo.ManulaGolikipa huyo namba moja wa klabu ya Simba amekua nje ya uwanja kwa muda mrefu akiwa anauguza majeraha ya goti ambayo yamemueka nje ya uwanja kwa takribani miezi mitatu sasa.

Mashabiki wa klabu ya Simba wamefurahia kwa kiwango kikubwa habari kutokana na ubora wa golikipa huyo ambao amekua nao, Lakini pia kutokana na magolikipa ambao wamekua golini mwa Simba kushindwa kuvaa viatu vya kipa huyo ipasavyo.ManulaGolikipa Aishi Manula kama amefanikiwa kuanza mazoezi ya pamoja na wachezaji wenzake ni wazi kua anaweza kuanza kucheza michezo ya klabu hiyo siku za hivi karibuni jambo ambalo mashabiki wa klabu hiyo walikua wanalisubiri kwa hamu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.