Winga wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Brazil Antony Santos hataondoka ndani ya klabu hiyo kwa uhamisho wa jumla wala mkopo kama ambavyo inataarifiwa.

Manchester United hawana mpango wa kumuachia Antony na ataendelea kua moja ya wachezaji muhimu ndani ya kikosi cha Man United, Ni wazi winga huyo anahitajika na klabu hiyo haswa kocha wake Erik Ten Hag.antonyTaarifa mbalimbali zilikua zinaeleza winga huyo anaweza kurudi klabu ya Flamengo ya Brazil kwa mkopo, Lakini Man United imekanusha taarifa hizo na kusema hawana mpango wa kuondoka klabuni hapo.

Winga Antony alihusishwa na kujiunga na klabu ya Flamengo ya kwao Brazil haswa wakieleza anaweza kua kwenye dili la mabadilishano baina yake na mshambuliaji wa Flamengo Gabriel Barbosa.antonyWinga huyo amekua hana muendelezo wa kiwango kizuri ndani ya timu hiyo jambo ambalo limefanya tetesi kuibuka kua anaweza kuondoka klabuni hapo, Lakini taarifa zinaeleza kua klabu hiyo haina mpango wa kuachana na winga huyo.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa