Klabu ya soka ya Simba bado haijaonekana kurudia kwenye utimamu wake baada ya kupokea kichapo cha mabao matano kwa moja kutoka kwa wapinzani wao wa jadi klabu ya Yanga.
Simba leo imeangusha alama tena mbele ya klabu ya Namungo baada ya kulazimishwa sare ya bao moja kwa moja wakiwa katika mchezo wa NBC uliopigwa katika dimba la Uhuru jijini Dar-es-salaam.Wekundu wa Msimbazi walianza mchezo wakioneakana kushambulia kwajili ya kupata bao la mapema, Lakini ni Namungo ambao walifanikiwa kupata bao la kuongoza kupitia kwa mshambuliaji wake Reliants Lusajo na kwenda mapumziko wakiongoza bao moja.
Kipindi cha pili Mnyama alionekana kuja na kasi kwajili ya kupata bao la kusawazisha na hata kupata la ushindi, Lakini Nmaungo walionekana kuzuia vizuri sana mpaka pale dakika ya 75 Jean Baleke kusawazisha bao kwa upande wa Mnyama.Klabu ya Simba walionekana kutafuta bao la ushindi kwa udi na uvumba lakini mambo hayakwenda kama wanavyotaka, Kwani mchezo ulimalizika kwa sare ya bao moja kwa moja na hii inaonesha mitaa ya Msimbazi bado haijatulia wakidondosha alama tano katika michezo miwili.