Winga wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Uingereza Jadon Sancho anatarajiwa kutimka ndani ya klabu hiyo kwenye dirisha dogo la mwezi Januari.

Sancho amekaa nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili sasa kutokana na kupishana na kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag na kugomea kuomba radhi kwa kocha jambo linalomfanya kuwepo nje ya uwanja mpaka sasa.sanchoWinga huyo alipishana na kocha wake na kuhitajika kuomba radhi kwa kocha wake ili aweze kurejea kwenye timu hiyo, Lakini winga huyo alishindwa kufanya hivyo kwa kilichodaiwa kua winga huyo anaona hastahili kuomba msamaha kwakua yeye ndio alikosewa.

Mchezaji huyo sasa anatarajiwa kuondoka ndani ya timu hiyo kutokana na kushindwa kujishusha kwa kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag, Huku ikielezwa klabu imeridhia mchezaji huyo aondoke klabuni hapo baada ya kuonesha vitendo vya utovu wa nidhamu.sanchoKlabu ya Borussia Dortmund ambayo amewahi kupita Jadon Sancho ndio timu ambayo winga huyo anahusishwa kutimkia katika dirisha dogo la mwezi Januari, Lakini mpaka sasa haijathibitika kama ataenda klabu hiyo lakini kuna uhakika wa mchezaji huyo kutimka mwezi Januari.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa