Sancho Aendelea Kukalia Kuti Kavu Man United

Winga wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza Jadon Sancho anaendelea kukalia kuti kavu ndani ya klabu hiyo kutokana na sakata lake dhidi ya kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag.

Sancho amekua nje ya uwanja kwa takribani mwezi sasa kutokana na kupishana na kocha wake baada ya mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya klabu ya Arsenal ambapo Man United walipoteza kwa mabao matatu kwa moja.sanchoWinga huyo wa kimataifa wa Uingereza mpaka sasa inaonekana kesi imeelemea upande wake, Kwani taarifa kutoka vyanzo vya ndani ya klabu ya Manchester United vinaeleza uongozi wa klabu hiyo upo pamoja na kocha wa timu hiyo.

Mchezaji huyo alitakiwa kuomba msamaha juu ya kitendo alichokifanya mwezi mmoja uliopita cha kumpinga kocha wake hadharani, Lakini mchezaji mpaka sasa imeonekana amegoma kuomba radhi jambo ambalo linaendelea kumuweka nje ya uwanja.sanchoMagwiji mbalimbali wa zamani wa klabu hiyo kama Roy Keane, Rio Ferdinand, pamoja na Dimitar Berbetov wakimtaka Jadon Sancho kuomba radhi kwani mwisho wa siku mchezaji hataweza kushinda mbele ya kocha na ni wazi kocha anapewa ushirikiano na uongozi wa klabu hiyo.

Acha ujumbe