DODOMA, ARUSHA KUJENGWA VIWANJA VYA KISASA

KATIBU wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo, Gerson Msigwa amesema Viwanja viwili vya Dodoma pamoja na Arusha vinavyotarajiwa kujengwa vitakuwa na uwezo wa kubeba watazamaji Elfu 30 kila kiwanja.

Msigwa alisema, mradi wa viwanja hivyo utaanza haraka sana na vitakuwa vya kisasa ili kuendana na hadhi ya mashinano na matakwa ambayo Caf wanataka.dodomaAkizungumzia mipango hiyo Msigwa alisema: “Viwanja ambavyo Rais ameagiza tufanye utekelezaji wake wa kuvijenga pale Dodoma na Arusha vitakuwa na uwezo wa kubeba mashabiki Elfu 30 kwa kila uwanja mmoja.

“Lakini pia muda huo huo tutajenga viwanja kadhaa vya mazoezi ili kukamilisha maandalizi kikamilifu, utekelezaji wake umeshaanza mara moja na tutamaliza ujenzi ndani ya wakati pamoja na ule ukarabati mkubwa wa uwanja wa Benjamin Mkapa na ule wa Amani visiwani Zanzibar.

“Niwahakikishiea vitakuwa na muonekano wa kisasa na wenye kumpendeza kila mtu na utakuwa na hadhi ya kimataifa kama ambavyo ilivyo kwenye nchi nyingi duniani ambazo zimeendelea kisoka,” alisema.dodomaJana, Caf waliitangaza Tanzania kwa kushirikiana na mataifa ya Uganda na Kenya, kuwa yamepata nafasi ya kuandaa mashindano ya Afcon, yanayotarajiwa kufanyika mwaka 2027.

Acha ujumbe