Sancho Kaondolewa Timu ya Kwanza

Winga Jadon Sancho aondolewa kwenye timu ya kwanza ya Manchester United na ataendelea kufanya mazoezi binafsi mpaka pale ambapo suala lake la utovu wa nidhamu litamalizwa.

Taarifa iliyotoka dakika chache kutoka Manchester United imeeleza winga Jadon Sancho ataendelea kufanya mazoezi ya peke yake na hatajumuika na timu ya kwanza akisubiri suala lake la nidhamu kupatiwa ufumbuzi.sanchoWinga Jadon Sancho aliingia kwenye mvutano na kocha wake Erik Ten Hag siku kadhaa zilizopita kutokana na kauli ya kocha huyo baada ya mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya klabu ya Arsenal ulioisha kwa Man United kupoteza.

Kocha Ten Hag alieleza kua mchezaji Jadon Sancho hakua hata kwenye sehemu ya kikosi kilichocheza dhidi ya Arsenal kutokana na mchezaji huyo kutokuonesha kiwango kizuri katika mazoezi jambo ambalo winga huyo alikanusha na kuonesha utovu wa nidhamu.sanchoSiku moja nyuma winga huyo alifuta andiko lake aliloliweka kwenye mtandao wake wa kijamii wa X zamani ukifahamika kama Twitter akimshutumu kocha wake, Baada ya kushusha andiko hilo ilitafsiriwa kama matatizo yamamelizika kumbe suala bado halijamalizika.

Acha ujumbe