Winga wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Uingereza Jadon Sancho yuko mbioni kukaa kikao na kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag kwajili ya kumaliza mgogoro unaoendelea baina yao.
Winga Jadon Sancho inafahamika hayupo kwenye mawasiliano mazuri na kocha Erik Ten Hag tangu klabu hiyo ipokee kipigo cha mabao matatu kwa moja dhidi ya klabu ya Arsenal katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza.Inafahamika kua kocha Erik Ten Hag alieleza kua winga huyo hakua sehemu ya kikosi katika mchezo dhidi ya Arsenal kutokana na kutokuonesha kiwango bora katika mazoezi ya klabu hiyo jambo ambalo winga huyo raia wa kimataifa wa Uingereza alikanusha hadharani.
Baada ya tukio hilo la majibizano baina ya mchezaji na kocha wa klabu ilileta picha ya tofauti sana nje ya klabu hiyo, Hivo mchezaji huyo na kocha wake wanaelezwa wako mbioni kukaa mezani ili kumaliza tofauti zao.Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kocha na mchezaji wake wako mbioni kukaa ili kumaliza tofauti zao, Lakini sio jambo ambalo linaweza kufanyiwa maamuzi tu ya siku moja kwani Sancho alifanya kitendo kikubwa cha utovu wa nidhamu.