Sancho Haendi Saudia Arabia

Winga wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza Jadon Sancho inaelezwa hana mpango wa kutimkia Saudia katika klabu ya Al Ettifaq kama ambavyo taarifa zilikua zimesambaaa.

Upande wa klabu umekanusha taarifa hizo pamoja upande wa mchezaji Jadon Sancho na kuelezwa hakuna mazungumzo yeyote yanayoendelea kumuhusu mchezaji huyo kutimkia klabu ya Al Ettifaq ya nchini Saudia Arabia.sanchoTaarifa mbalimbali zilikua zikienea kumuhusu mchezaji huyo raia wa kimataifa wa Uingereza kua anaondoka klabuni hapo, Huku hii ikisababishwa na mchezaji huyo baada ya kupishana na kocha wake Erik Ten Hag.

Winga huyo raia wa kimataifa wa Uingereza alitoa taarifa kwa umma siku ya jumapili akipinga kauli ya kocha wake ambaye alisema mchezaji huyo hakua sehemu ya kikosi kilichocheza dhidi ya Arsenal kutokana na kutokuonesha uwezo mkubwa mazoezini.sanchoJadon Sancho na kocha Ten Hag pamoja na jopo zima la makocha wanaelezwa watakaa mezani siku za usoni kwajili ya kumaliza tofauti zao kutokana na ambacho kimetokea baina ya mchezaji huyo na kocha wake siku ya jumapili.

 

Acha ujumbe