Al Ittihad Yambeba Luiz Felipe

Klabu ya Al Ittihad inayoshiriki ligi kuu nchini Saudia Arabia yaendelea kufanya usajili kutoka barani ulaya kwani wamefanikiwa kukamilisha usajili wa beki wa klabu ya Real Betis kutoka nchini Hispania Luiz Felipe.

Klabu ya Al Ittihad imefanikiwa kumsajili beki huyo kwa kiasi cha euro milioni 25 kwa beki huyo wa kimataifa wa Italia mwenye asili ya Brazil na sasa atakipiga katika ligi kuu nchini Saudia.luiz felipeTimu kutoka nchini Saudia zimeendelea kua tishio kwa vilabu mbalimbali kutoka barani ulaya kwani beki Luiz Felipe ni beki mwenye umri mdogo wa miaka 26 tu, Lakini ameweza kuondoka ulaya na kujiunga na ligi kuu nchini Saudia jambo ambalo ni geni.

Timu mbalimbali kutoka barani ulaya ziliamini kua vilabu kutoka nchini Saudia vitakua vinasajili wachezaji ambao umri umesogea kama ilivyokua China miaka kadhaa iliyopita, Lakini kwa Saudia imekua tofauti kwani wao wanasajili hadi wachezaji wenye umri mdogo.luiz felipeKlabu ya Al Ittihad ni moja ya vilabu ambavyo vimefanya usajili mkubwa sana kutoka barani ulaya katika dirisha hili kubwa kwani mbali na Luiz Felipe, Lakini pia walifanikiwa kumsajili mshindi wa Ballon Dor mwaka 2022 Karim Benzema na aliyekua kiungo wa klabu ya Liverpool Fabinho.

Acha ujumbe