Musiala Kuwakosa Japan na Ufaransa

Mchezaji nyota wa klabu ya Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani Jamal Musiala amejitoa kwenye timu ya taifa ya Ujerumani kutokana na majeraha ya mgongo ambayo yamempata.

Jamal Musiala atawakosa Japan na Ufaransa katika mchezo wa kirafiki baina ya Ujerumani na timu hizo mbili kutokana na kile kinachoelezwa ni majeraha ambayo yamempata mchezaji huyo fundi na tegemezi wa klabu ya Bayern Munich.musialaMchezaji huyo alikosekana katika michezo miwili ya mwisho ya klabu yake ya Bayern Munich kutokana na kuandamwa na majeraha ya misuli ya paja, Lakini alirudi mazoezini mapema wiki hii na taarifa mpya zinaeleza amepata majeraha mengine ya mgongo.

Taarifa ya Bayern Munich imetoka leo na kueleza kua mshambuliaji huyo hatajiunga na na timu ya taifa ya Ujerumani kama ambavyo ilipangwa na atakosa michezo ya kirafiki baina ya Japan na Ufaransa kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya mgongo.musialaMshambuliaji Jamal Musiala hajaanza msimu vizuri kutokana na kuandamwa na majeraha ya hapa na pale. Lakini mchezaji huyo amekua msaada mkubwa wa klabu ya Bayern kutokana na ubora mkubwa aliokua nao na jana akitajwa tena kuwania tuzo ya mchezaji bora kijana wa dunia.

 

Acha ujumbe