Manchester United Kushirikiana na Getafe

Klabu ya Manchester United ina mpango wa kushirikiana na klabu ya Getafe kama mchezaji wao aliye kwa mkopo klabuni hapo Mason Greenwood atafanya vizuri ndani ya klabu hiyo.

Manchester United wanataka kuifanya Getafe kama sehemu ambayo wachezaji wao watakua wanaongeza ubora ubora kama wachezaji wanaotoka akademi ya klabu hiyo na wengine ambao hawapati mda wa kutosha klabuni hapo.manchester unitedMpango huu unaweza kua na faida kwa klabu ya Getafe kwani watakua wanapata wachezaji wazuri kutoka Man United jambo ambalo kwao litakua na faida kubwa kwani Getafe kupata mchezaji kutoka Man United ni jambo kubwa kwao.

Man United wamemtoa kwa mkopo mchezaji wao Mason Greenwood kuelekea klabu ya Getafe ya nchini Hispania jambo limekua jema kwa klabu hiyo na ndio sababu ya United kutaka kulipa fadhila kwa Getafe endapo mkopo wa mchezaji huyo utaenda vizuri.manchester unitedManchester United inaamini klabu ya Getafe itakua sehemu sahihi sana kwa wachezaji wao ambao watakua wanahitaji kuboresha uwezo wao kama tu mkopo wa Greenwood utaenda vizuri kunako klabu hiyo kutoka nchini Hispania.

Acha ujumbe