Winga wa klabu ya Arsenal raia wa kimataifa wa Ivory Coast Nicolas Pepe kutimka Arsenal na kuelekea nchini Uturuki katika klabu ya Trabzonspor baada ya kukataa ofa za Saudia.
Nicolas Pepe mpaka sasa inafahamika kua hayupo kwenye mipango ya klabu ya Arsenal, Hivo klabu hiyo imeamua kumuachia na winga huyo yuko mbioni kuondoka klabuni hapo na kuelekea nchini Uturuki.
Arsenal wanaelezwa kua wapo kwenye hatua za mwisho kumalizana na winga huyo ambaye walimtoa kwa mkopo msimu uliomalizika katika klabu ya Nice kwakua mchezaji huyo hayupo kwenye mipango ya kocha wa klabu hiyo.
Winga huyo alijiunga na klabu ya Arsenal mwaka 2019 kwa ada kubwa ya uhamisho lakini hakufanikiwa kuonesha makali ndani ya timu hiyo mpaka kufikia kutolewa kwa mkopo msimu uliomalizika na klabu hiyo kuamua kumuachia kwasasa.
Vilabu kadhaa kutoka nchini Saudia vinaelezwa vilionesha kumuhitaji mchezaji huyo lakini Pepe ameonesha kua hakuvutiwa kujiunga na vilabu hivo huku yeye akitoa kipaumbele kwa klabu ya Trabzonspor ya nchini Uturuki.

