Modric Hapendezwi Kukaa Benchi Madrid

Kiungo wa klabu ya Real Madrid Luca Modric ameonesha kua hapendezwi na hali ya kukaa benchi ndani ya klabu hiyo hii ikiwa imekuja baada ya mchezaji huyo kutokupata muda wa kucheza zaidi ndani ya timu hiyo.

Luca Modric amesema ameshangazwa na yeye kukaa benchi michezo mitatu mfululizo jambo ambalo halijawahi kutokea tangu ajiunge na klabu hiyo mwaka 2012 lakini akieleza hayo ni maamuzi ya kocha zaidi.modricKiungo huyo raia wa kimataifa wa Croatia ambaye ambaye ameongeza mkataba wa mwaka mmoja ndani ya klabu hiyo amesema yeye kuwepo ndani ya klabu ya Real Madrid hayupo tu bali anahitaji kucheza na kufurahi japo amesema anaelewa kipaumbele zaidi ni timu kuliko mtu mmoja.

Kiungo huyo amesema ana mahusiano mazuri na kocha wa klabu hiyo na hakuna hisia zozote mbaya kwani kocha huyo alizungumza nae na kumueleza wanapaswa kupambania nafasi kwakua eneo la kiungo la klabu hiyo lina ushindani mkubwa na vijana waliopo klabuni wana ubora mkubwa.modricLuca Modric pia ameeleza anatambua uwezo waliokua nao wachezaji vijana ndani ya timu hiyo na kusema watahitaji kujifunza mambo mengi kutoka kwao kama wakongwe, Hivo yupo tayari kuwaelekeza vijana hao hadi pale ambapo watachukua nafasi moja kwa moja ndani ya timu hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.