Italia Kibaruani Dhidi ya Ukraine Leo

Timu ya taifa ya Italia leo itakua na kibarua katika mchezo dhidi ya timu ya taifa ya Ukraine wa kufuzu michuano ya mataifa ya ulaya mwaka 2024 itakayofanyika nchini Ujerumani.

Timu ya taifa ya Italia ambao ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo watahitaji kushinda mchezo wa leo ili kufufua matumaini ya kushiriki michuano hiyo mwaka ujao na kuweza kuitetea pia.italiaKikosi hicho chini ya kocha Spalletti kiko kwenye hali mbaya kwani mpaka sasa wanakamata nafasi ya tatu kwenye kundi lao ambapo wamefanikiwa kukusanya alama 4 mpaka sasa kwenye jumla ya michezo mitatu ambayo tayari wameicheza.

Mabingwa hao watetezi wanahitaji kupambana zaidi ili kurudisha matumaini ya kutetea taji lao mwakani, Kwani bila kufuzu hawataweza kupata fursa ya kuweza kutetea taji lao hivo jambo la msingi ni kuweza kufuzu kwanza.italiaKocha Luciano Spalletti ambaye aliiongoza klabu ya Napoli kutwaa ubingwa wa Italia msimu uliomalizika ndio amepewa jukumu la kuinoa timu hiyo, Huku wengi wakiwa na matumaini makubwa kua kocha huyo anaweza kuirudisha Italia inayofahamika.

Acha ujumbe