Klabu ya Manchester United inaelezwa ipo kwenye mpango wa kumuongezea mkataba winga wake kinda raia wa kimataifa wa Uruguay Facundo Pellistri.

Winga Pellistri amekua hapati nafasi ya kuanza mara kwa mara ndani ya kikosi cha Manchester United, Lakini kila anapopata nafasi amekua akionesha ubora jambo ambalo limewafanya mabosi wa klabu hiyo kufikiria kumuongezea mkataba.manchester unitedMkataba wa winga huyo unamalizika mwaka 2025 lakini Man United wameandaa ofa ya kumpa mkataba wa muda mrefu mchezaji huyo wa kimataifa wa Uruguay mwenye umri wa miaka 21 tu.

Manchester United wanaamini Pellistri ni miongoni mwa vipaji maridhawa ambavyo wanavimiliki klabuni hapo na ndio sababu wanataka kuchangamkia fursa ya kumpa mkataba mpya wa muda mrefu ambao utaendelea kumfunga klabuni hapo.manchester unitedWinga huyo amewahi kutolewa kwa mkopo mara kadhaa kwenda klabu ya Deportivo Alaves ya nchini Hispania, Huku taarifa zikieleza pia alitakiwa kutolewa kwa mkopo tena msimu huu lakini kocha Ten Hag akaamua abaki klabuni hapo na kuahidi kumpa muda wa kucheza zaidi.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa