Cancelo: Ndoto Yangu ilikua kucheza Barca

Aliyekua beki wa klabu ya Manchester City raia wa kimataifa wa Ureno Joao Cancelo amefunguka na kusema ndoto yake ilikua siku moja kuicheza klabu ya Barcelona ya nchini Hispania.

Beki Cancelo amejiunga na klabu ya Barcelona kwa mkopo wa mwaka mzima mpaka msimu huu utakapomalizika amesema ndoto yake ilikua kuwatumikia mabingwa wa soka nchini Hispania kwasababu anataka kuwaonesha watu walioamini juu yake kua sio rahisi kucheza Barca.CanceloBeki huyo wa zamani wa Juventus anasema hiyo ilikua ni ndoto ambayo alikua akiiota tangu akiwa kijana mdogo, Huku akiongeza marafiki zake wote wanatambua kua wachezaji ambao wamekua kioo kwake wote wamecheza Barcelona.

Beki huyo ambaye aliitumikia klabu ya Bayern Munich msimu uliopita kwa mkopo pia akitokea Man City ameenda sambamba na Mreno mwenzake Joao Felix ambaye nae amejiunga na Barcelona kwenye dirisha hili na kusema ndoto yake imetimia.CanceloBarcelona wamemchukua beki Cancelo wakiamini watapata ubora mkubwa kutoka kwa beki huyo katika upande wao wa kulia ambao alikua akicheza beki Sergio Roberto na Julias Kounde ambaye kiasili sio beki wa pembeni, Hivo Barca wanaamini beki huyo atawapa ubora ambao wanaoutarajia.

Acha ujumbe