Kocha Tottenham Amsifia Beki Romero

Kocha wa klabu ya Tottenham Hotspurs Ange Postecoglou amesema asingependa kukabiliana na beki wa timu raia wa kimataifa wa Argentina Cristian Romero akiwa timu tofauti.

Kocha huyo wa Tottenham amesema beki huyo amekua akionesha ubora wa hali ya juu toka akiwa mazoezini jambo ambalo analihamishia mpaka kwenye mechi kitu ambacho kiamvutia kocha huyo.TottenhamKocha huyo anasema vijana wengi mazoezini hawapendi kukabiliana na Cuti Romero kwani amekua mchezaji mgumu zaidi kukabiliani nae hata ikiwa katika kiwanja cha mazoezu na ndio sababu kocha huyo amesema asingependa kukabiliana na beki huyo.

Mchezaji huyo amekua akionesha ubora mkubwa tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea Atalanta ya nchini Italia, Jambo ambalo limemfanya beki huyo kua moja ya wachezaji muhimu ndani ya timu hiyo.TottenhamBeki huyo amepokea sifa kutoka kwa kocha Ange kutokana na namna ambavyo amekua mfano wa kuigwa kwa wachezaji wenzake ndani ya Tottenham kutokana na namna ambavyo anaonesha juhudi kuanzia kwenye kiwanja cha mazoezi mpaka kwenye mechi.

Acha ujumbe