Cancelo na Barcelona ni suala la Muda

Beki wa klabu ya Manchester City na timu ya taifa ya Ureno Joao Cancelo dili lake la kwenda klabu ya Barcelona limekaribia kumalizika ili aweze kujiunga na mabingwa hao kutoka nchini Hispania.

Joao Cancelo alishamalizanma na Barcelona katika maslahi binafsi na alionesha kua anataka kujiunga na klabu hiyo,Hivo anachokisubiri kwasasa ni klabu yake kuidhinisha yeye kujiunga na mabingwa hao wa Hispania kuanzia sasa.CanceloKlabu ya Barcelona walikua wanahitaji kwa kiwango kikubwa beki wa upande wa kulia na beki huyo wa kimataifa wa Ureno alifanikiwa kua kipaumbele chao hivo mpaka sasa wamefikia kwenye hatua nzuri kukamilisha dili hilo.

Barcelona wamekubaliana na Manchester City kumchukua beki huyo wa kimataifa wa Ureno kwa mkopo wa msimu mzima na kipengele cha kumnunua jumla mwishoni mwa msimu huu.CanceloBeki Joao Cancelo anatolewa mkopo kwa mara ya pili ndani ya klabu ya Manchester City kwani msimu uliomalizika alitolewa kwa mkopo kwenda klabu ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani, Lakini msimu huu atatolewa kwa mkopo Barcelona na kipengele cha kumnunua kwa mkataba wa kudumu.

Acha ujumbe